Thursday, March 19, 2009

KISWAHILI VERSION !



Kwa Wapenzi wasomaji Wa .felismwambalo.blogspot.com
Bila shaka mtakuwa mmebarikiwa na taarifa mzipatazo kutoka kwenye page hii.
Wanaotumia lugha ya KISWAHILI, pia hatuja wasahau, ndio naana tunakuletea Sehemu ya Kishwahili...
Tutaanza na Somo Ambalo najuwa litakubariki linaloitwa
ROHO YA UPOLE
Upole ni moja kati ya tabia zinazo wapendeza watu. Upole hauna haraka ya kusema wala kuamua jambo, Upole unaunyenyekevu na usikivu.

Ipo tofauti kati ya Upole na ukimya; Si kila mpole ni mkimya na si kila mkimya ni mpole...

Roho ya Upole ni moja kati ya tabia za Mungu. Mungu wetu ni mpole, anawavumilia watu na
dhambi zao; na mapungu fu yao... Anatusisitiza kuwa na roho ya upole.

Imeandikwa hivi :

Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, usiondoke mara mahali ulipo. Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
Muhubiri 10 : 4

Mungu wetu ni mewnye hekima nyingi sana, katika ulimwengu wa Roho ambao sisi kwa jinsi ya rohoni tunaishi, hakuna mtawala, ila mmoja tu naye ni yeye Mungu aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote. Ila kwetu wanadamu wapo viongozi ambao wao hupokea maagizo yote kutoka kwa mtawala na kuyaleta kwetu.
Nasema huko kwenye ulimwengu wa mwili kunao watawala, tumeisha sikia wengi tu, na wana makeke mengi ru, wengine wanakula mpaka watu.
Imeandikwa :
" Liko baya linaonekana chini ya jua nalo ni kama kosa litokalo kwake atawalaye, hya kuwa Upumbavu huwekwa mahali pa juu sana; nao wakwasi hukaa mahali pa chini " (Mhubiri 10:5-6)
Ukisoma Biblia ya Kiingereza ule mstari wa sita (6) umeandikwa hivi " Stupid people are given positions of authority". (Wapumbavu wapewa nafasi katika mamlaka)
Bado nasema Mungu wetu ni Mungu wa hekima. Kwanini anazungumzia watawala katika biblia? Inawezekana anasema ilituweze kuwachukulia watawala tunaoishinao ambao hawajamjua Mungu. Lakini Pia inawezekana katika ulimwengu wa Roho, wakatokea watawala ambao roho anaepingana na Roho wa Mungu amewavaa bila wao kujua, anawatumia bila hao kujua. Badala ya kumuuliza Mungu katika maamuzi yao, wanatumia hekima zao wenyewe.
Tutaendelea...